• Breaking News

  Aug 22, 2016

  Usain Bolt aingia kwenye kashfa ya picha za mahaba na mwanafunzi


  wanariadha wa Jamaica, Usain Bolt (30) ameingia kwenye kashfa baada ya picha zake kadhaa akiwa na mwanafunzi wa kike wa Rio wa miaka 20 kusambaa mtandaoni.

  Mwanafunzi huyo ambaye ametambulika kwa jina la Jady Duarte alisambaza picha kadhaa kwenye mtandao wa Whatsapp akiwa na Bolt kwenye pozi mbalimbali za kimahaba huku picha nyingine zikiwaonyesha wakiwa kwenye klabu ya usiku ya Barra de Tijuca iliyopo jijini Rio de Janeiro.


  Akiongea na gazeti la Extra, Duarte amedai kuwa hakuwa anafahamu kama mwanariadha huyo ni maarufu zaidi duniani ndio maana ikawa rahisi kwake kusambaza picha hizo.


  Aidha Bolt anadaiwa kuwa na mahusiano na Kasi Bennett (26) kwa takribani miaka miwili sasa na tayari walikuwa kwenye mikakati ya kufunga ndoa.

  Hata hivyo hayo yakiendelea kutokea Bolt anasherehekea kusaini dili jipya na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike kwa mkataba wa miaka 10 ambao atakuwa akiingiza kiasi cha dola milioni 30 kila mwaka akiungana na mcheza kikapu, Kevin Durant aliyesaini na kampuni hiyo mwaka 2014.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku