• Breaking News

  Aug 18, 2016

  Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, Lakini Chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

  Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba, nawashauri kwa dhati kabisa, tafadhalini sana msiandamane, na kusitisha hiyo Operesheni UKUTA, ili kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, na sio tuu ana nguvu zaidi yako, na tayari, umeishajua ni dikiteta, bali ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.

  Misingi ya Katiba na The Rule of Law 
  Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of law) ambapo inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!.

  The Separation of Powers & Check and Balance .
  Nchi yetu ina mihimili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii mitatu, ilipaswa kufanya kazi kwa kujitegemea bila mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine (independence), huki kila mhimili uki act as a watchdog wa muhimili mwingine usivuke mipaka ya madaraka au mamlaka yake yaani (The sepaation of powers check and balance).

  Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.

  Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu mihimili yao. President ndio mkuu wa the executive, Spika ndio mkuu wa The Legistlatue, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja na nia njema kuwa mihimili yote inamamlaka na hakuna mhimili wowote uliokuwa unapaswa kuwa na mamlaka kuliko mhimili mwingine, lakini kiukweli, mhimili wa the executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa the executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!.

  Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
  Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba, mhimili wa Bunge na Mahakama ilipaswa kuingilia kati kwa kumcheck mkuu wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais ajisikie kuwa he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always right!".

  Udikiteta wa Magufuli.
  Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni dikiteta wa ukweli ambaye hana msalie mtume, na alipoingia tuu madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali, likiwemo bunge na mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge wakapige magoti kwa rais kuomba kutimiza wajibu wao!.

  Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa kujisubmit chini ya the executuve, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama, lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive, hivyo kumfanya rais ndio kila kitu!.

  Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama, wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!.

  Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli ni dikiteta mzalendo!, mwenye uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia uchumi wa gesi na viwanda.

  Mungu mbariki Magufuli!.

  Mungu ibariki Tanzania.

  Wasalaam.

  Pasco/Jamii Forums

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku