Aug 9, 2016

Utafiti Waonyesha Kweli Supu ya Pweza Inaongeza Hamu ya Kufanya Mapenzi


Wafamasia katika Chuo Kikuu cha Muhimbili wamedai wamethibitisha kisayansi kuwa supu ya pweza inaweza kuchochea hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume.
Kwa miaka mingi ilikuwa ikiaminika na watu wengi hasa wa ukanda wa pwani ya Tanzania na Afrika Mashariki kuwa supu hiyo inaongeza hamu ya kufanya mapenzi lakini kulikuwa hakuna uthibitisho wa kisayansi wa kuunga mkono madai hayo

''Sio kitu cha imani tena, sasa hivi tuna ushahidi wa awali unaotupa mwanga wa matumaini kuthibitisaha matokeo hayo katika mwili wa binadamu kwa utafiti zaidi'' 

alisema Profesa Eliangiringa Kaale mkuu wa kitengo cha utafiti na ukuzaji wa maabara katika Chuo Kikuu cha Muhimbili shule ya Famasia ambaye pia alishiriki kusimamia utafiti huo.

Utafiti huo ulifanywa na wanafunzi na wasimamizi wa famasi kwa panya dume.
Hata hivyo Profesa Kaale alionya wanywaji wa supu ya pweza kuwa matokeo ya utafiti huo hayamaanishi kuwa tiba ya kuponyesha matatizo ya kushindwa kufanya ngono kwa wanaume imepatikana


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR