• Breaking News

  Aug 10, 2016

  Uturuki yaitahadharisha Tanzania Juu ya Ugaidi

  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Yasemin Eralp
  Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania umeonya juu ya udhamini unaotolewa na kundi lenye mrengo wa kigaidi la FETO linaloelezwa kuhusika moja kwa moja na mashambulizi ya kigaidi mwezi Julai mwaka huu jijini Instanbul.


  Yasemin Eralp ni balozi wa Uturuki nchini Tanzania ambaye kwa mara ya kwanza ameviita vyombo vya habari katika ubalozi wa nchi hiyo kuelezea hali halisi ya amani nchini Uturuki na usalama wa raia wa nchi nyingine waliopo katika nchi hiyo huku akibeba ujumbe wa kutaka nchi nyingine hasa za Afrika kuwa waangalifu na udhamini hususani wa elimu unaotolewa na kundi la FETO ambayo pia inadhamini baadhi ya taasisi za elimu nchini Tanzania.

  Aidha Balozi huyo ameeleza kuwa kwa sasa nchi hiyo imefunga taasisi zote za elimu vikiwemo vyuo vikuu vinavyodhaminiwa na FETO nchini Uturuki lakini inafanya utaratibu wa kuwahamishia wanafunzi waliokuwa katika vyuo hivyo katika taasisi nyingine kuendelea na masomo yao kwa kupata taarifa sahihi kutoka katika nchi zao ili taratibu hizo ziendelee.

  Balozi Yasemin amesema kuwa taratibu nyingine zote za kidiplomasia baina ya nchi hiyo na nchi nyingine duniani ikiwemo Tanzania, zinaendelea vizuri huku akieleza kuwa hali ya usalama inaendelea kuimarika nchini humo hasa jijini Instanbul.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku