• Breaking News

  Aug 4, 2016

  Vanessa Mdee ajibu tuhuma za Timbulo kuwa alimpigia simu kutaka collabo akamwambia hamjui

  Muimbaji wa ‘Ngomani’ Timbulo amesikika kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV akimtupia lawama Vanessa Mdee kuwa alimpigia simu kumuomba amshirikishe kwenye wimbo wake lakini akamweleza kuwa hamjui.

  Amedai kuwa kitendo hicho kilimnyong’onyeza kwa kuona kuwa ni kama muimbaji huyo amemletea pozi ilhali ana uhakika kuwa atakuwa anamfamu.

  Nimemtafuta Vanessa kumuuliza kuhusu malalamiko hayo ya Timbulo na alikuwa na haya ya kusema:

  “Kusema kweli sikumaanisha kumdharau au kumwonesha kwamba simfahamu Timbulo bali siku zote mtu akiwa anakupigia na namba hauna kitu cha kwanza utauliza ‘haloo haloo, nani mwenzangu’ akasema Timbulo, nikasema ‘Timbulo nani?’ sikumaanisha kwa ubaya lakini kama amechukulia kwa ubaya naomba anisamehe na I hope everything is cool and I wish him all the best.”

  Timbulo pia alimtupia lawama Malaika kuwa alimletea mapozi licha ya kumsaidia sana kipindi ambacho hajulikani.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku