• Breaking News

  Aug 30, 2016

  Video: Beyonce Ssababisha Rapper wa Marekani Kuvunja Mahojiano Baada ya Kumgusa

  Hata ukiwa unajiona wewe ni muongeaji sana lakini siyo pale utakapokutana na Beyonce – unaweza ukageuka bubu kwa muda.

  Kilichomtokea rapper wa Chicago, Chance the Rapper wikiendi hii kwenye backstage ya tuzo za MTV VMA lazima atakiweka kwenye kumbukumbu ya maisha yake kwa kuwa watu wengi wanatamani kiwatokee.

  Wakati Chance the Rapper akihojiwa na mtangazaji wa MTV, Meredith Graves kuna mtu alikuja nyuma ya rapper huyo na kumlalia kwenye upande wa bega lake la kushoto alipogeuka alishangaa kumuona ni Beyonce aliyefanya kitendo hicho.

  Ilikuwa ni kama ndoto kwa rapper huyo alijikuta akimkumbatia malkia huyo na kushindwa kumwambia chochote na hata interview ikaishia hapo huku akimalizia kwa kusema “This is my life.”

  Hata Dj Khaled aliwahi kuliambia gazeti la The New York Times kuwa heshima aliyonayo kwa Bey ni kubwa mno kiasi cha kuwa muoga wa kuongea sana akiwa naye ili asije akaharibu.

  Queen Bey aliongoza kwa kuchukuwa tuzo nane katika vipengele 11 alivyokuwa amewekwa kwenye tuzo hizo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku