• Breaking News

  Aug 3, 2016

  VIDEO: Ndege ya Emirates Yatua Kwa Dharura Dubai Baada ya Kushika Moto Angani

  Ndege ya kampuni ya Emirates imeripotiwa kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai, baada ya kushika moto ikiwa angani, serikali ya Dubai imethibitisha kuwa ndege ya Emirates aina ya Boeing 777-300 imetua Dubai ikiwa na abiria na watumishi wa ndege 300.

  Ndege hiyo aina ya Boeing 777-300 rubani alijua kuwa ina tatizo masaa matatu baada ya kupaa ikitokea uwanja wa ndege wa Trivandrum India na kutoa signal ya kuomba kutua kwa dharura, hadi sasa taarifa kutoka mirror.co.uk inaripoti kuwa hakuna mtu aliyeripotiwa kuumia.

  Emirates na wataalamu wao bado hawajajua nini chanzo kilichosababisha ndege hiyo kushika moto, taarifa kutoka kwa msemaji wa Emirates inaeleza “Emirates inathibitisha kuwa ndege yao imepata ajali Dubai ikiwa inatokea India, ndege ilikuwa na abiria 282 na wafanyakazi 18 imetua kwa dharura dubai baada ya kushika moto”

  Video:

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku