• Breaking News

  Aug 27, 2016

  Video: Salama Jabir atoa ufafanuzi kuhusu Show ya Mkasi

  Salama Jabiri
  Mashabiki wa kipindi kilichoshinda tuzo mbili kwenye Tuzo za watu (2014 na 2015), MKASI, wamekuwa wakiuliza bila kupata majibu iwapo kitarudi tena baada ya Salama Jabir kuja na kipindi kipya, Ngaz Kwa Ngaz.

  “Mkasi ni kipindi kizuri, na nashukuru unaposema kuwa unakikubali lakini tumeamua kukipumzisha wakati bado kiko juu,” Salama alimuambia mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Lil Ommy wiki iliyopita.

  “Unajua TV ni kitu kikubwa sana sio kitu easy kama tunavyofikiria, ndio maana sometimes watu wanaanzisha vitu halafu wanashindwa ku-maintain. So sisi tumeamua kuipumzisha Mkasi wakati bado inafanya vizuri. Halafu kuna hizi issue za kuiganaigana sana, it bothers me pamoja na washkaji zangu.”

  Salama alisisitiza kuwa yeye na timu yake wameamua kuacha waone wengine wanafanya nini kwanza kabla ya kuamua kama itarudi ama kitapigwa chini kabisa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku