Marcus Rashford Baada ya Kufunga Goli
Goli la dakika za jioni liliihakikishia Manchester United pointi tatu nyingine katika mchezo wao wa tatu tangu kuanza kwa ligi ya EPL na hatimaye kuwa na pointi 9 kwenye kapu lao.

Marcus Rashford alikuwa shujaa wa mechi hiyo ya mwisho kati ya mechi nane zilizopigwa Agosti 27, Manchester ilikuwa ugenini kwenye uwanja wa Kingston Communications ikipambana na Hull City.

United inaendelea kukimbizana na Chelsea kileleni mwa ligi baada ya timu hizo kucheza mechi tatu na kushinda zote huku zikisubiri matokeo ya Manchester City yenye pointi 6 lakini ikiwa na mchezo mkononi.
Post a Comment

 
Top