• Breaking News

  Aug 4, 2016

  Vyuo Vitano Tanzania Vyafutwa..Orodha Hii Hapa

  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza kufunga na kuvifuta vyuo vitano kwenye orodha ya Vyuo vya Ufundi nchini, anaandika Pendo Omary.
   Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mhandisi Steven Mlote, Mwenyekiti wa NACTE amesema, hatua hiyo imefikiwa ili kutokana na kutokidhi viwango sambamba na kuboresha viwango vya elimu nchini.
  “Baraza limetengaza kuwa vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria vimepewa muda wa wiki mbili na kutakiwa vijisajili mara moja kwenye baraza hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
  “Vilevile, vibali vya usajili wa vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia ukomo hivyo vinapaswa kutekeleza masharti ya Usajili; wakati  vyuo 57 vimefikia ukomo wa ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya ithibati,” amesema.
  Mlote amesema, baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.
  “Vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria nimevipa muda wa wiki mbili vijisajili mara moja kwenye baraza kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria,” amesema.

  Vyuo vya Ufundi Vilivyofutiwa Usajili

  1. State College of Health and Allied Sciences – Dar es Salaam
  2. Zoom Polytechnic College – Dar es Salaam
  3. Tabitha College – Dar es Salaam (formerly: Thabita Vocational Training College – Dar es Salaam)
  4. Financial Training Centre – Dar es Salaam
  5. TMBI College of Business and Finance – Dar es Salaam

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku