Aug 17, 2016

Wasanii Orijino Komedi Wahojiwa, Washikiliwa Polisi

Jeshi la Polisi Dar leo limewahoji wasanii wa Orijino Komedi makosa ya kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii mwenzao Emanuel Mgaya “Masanja”.

Wasanii hao, Lucas Muhuvile maarufu Joti, Alex John “Mac Reagan” na Isaya Gideon “Wakuvanga” wamehojiwa leo sambamba na meneja wa kundi hilo, Sekioni David.

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Dar zinaeleza kuwa wasanii hao walikamatwa tangu jana jioni na kulala kituo cha Polisi hadi walipohojiwa juu ya tukio hilo.

Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinawaonesha wasanii hao wakiwa wamevalia sare zinazofanana na zile za Jeshi la Polisi wakiwa wanafanya gwaride, kama ishara ya kumpa heshima mwenzao, Emmanuel Mgaya “Masanja” aliyeachana na ukapera.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR