• Breaking News

  Aug 9, 2016

  Wastara Afunguka Kuhusu Kuwa na Ujauzito

  Msanii wa Bongo Movie Wastara Juma amepinga uvumi wa kutoka kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wanamzushia kwamba yeye ni mjamzito.

  Akiongea kwenye kipindi cha eNewz kinacho onyeshwa katika runinga ya EATV kila siku saa kumi na mbili, Wastara amewaambia wananchi kwamba tumbo la mimba hukua na halirudi ndani kwa hiyo waendelee kusubiri miezi tisa mpaka itimie kwani kwanzia waanze kusema yeye ni mjamzito ni miezi mine na tumbo haliendelei.

  Licha ya hilo Wastara amesema tumbo hilo ambalo walikuwa wanalihisi kuwa ni kijacho, ni kwamba aliridhika tuu na sehemu ambayo alikuwa, kwani alikuwa Msumbiji kibiashara kwa hivyo mazingira hayo yalimfanya kuwa na tumbo kubwa na hivi sasa yupo kwenye diet ili kupunguza mwili.

  "Unajua kinachonishangaza ni pale wale wanaposema mimi ni mjamzito na haelewi baba kijacho ni yupi kama ni yule wa ndoa ama ?," alisema Wastara Juma.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku