Aug 28, 2016

Watu Weusi ni 'Adui', Asema Gavana wa Marekani


Gavana wa jimbo la Maine nchini Marekani amesema kuwa watu wa rangi nyeusi ni 'adui' wa jimbo lake na kuonekana akipendekeza wapigwe risasi.

Akizungumzia kuhusu juhudi za jimbo la Maine kukabiliana na uhalifu wa dawa za kulevya,Paul LePage amesema kuwa adui mkubwa kwa sasa ni watu wenye rangi ama wale wa Hispanic.
''Wakati unapokwenda vitani,na adui anavaa nguo nyekundu na wewe unavaa nguo za rangi buluu ,unapiga risasi waliovaa nyekundu''.

Wanachama wakuu wa chama cha Democrat wamemtaka kujiuzulu.
Bwan LePage alitoa matamshi hayo alipokuwa akitaka kusahihisha matamshi aliyotoa hapo mbeleni yaliokosolewa kuwa ya kibaguzi.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR