Waziri Mkuu Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itahakikisha inalinda amani ya nchi kwa gharama zozote na kamwe haitoruhusu mwanasiasa yeyote kusababisha vurugu zitakazochochea uvunjifu wa amani.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kuwaondoa hofu wananchi kuwa serikali haitakubali mwanasiasa yeyote kuharibu amani.

“Ni kweli kuna viashiria, lakini nataka kukuhakikishia kwamba serikali tumesimama vizuri hatutaruhusu mwanasiasa yeyote atakaye sababisha vurugu nchi hii, kimbilio la katiba sijui tunaruhusiwa hapana hakuna jambo ambalo halina mipaka”,alisema Majaliwa.

Mheshimiwa Majaliwa alielezea kauli mbiu ya Rais amesema “kauli ya Rais Magufuli ya ‘hapa kazi tu’ ilikuwa sio neno la mchezo na kwamba lina maana kuwa watu wafanye kazi zinazowaletea tija.Post a Comment

 
Top