• Breaking News

  Aug 10, 2016

  Waziri Ummy Aishukia MOI

  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa siku 14 kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI) kuangalia matatizo yaliyopo na kuyafanyia tathmini, huku akisisitiza kambi za upasuaji zirejee na zianze kazi mara moja ifikapo Agosti 13, mwaka huu.

  Alisema bodi hiyo itakapokaa na kurudisha majibu kwake atafanya maamuzi likiwamo suala la uteuzi wa mkurugenzi wa taasisi hiyo, akisema imekaimiwa kwa kipindi kirefu na sasa ni wakati wa kumpata wa kuishikilia.

  “Kitu kinachonisumbua kichwa kwa sasa ni kuhusiana na kambi za upasuaji, naomba zianze kazi mara moja, wanaoteseka ni wananchi wa hali ya chini maana baada ya kufutwa kambi za upasuaji ikaanzishwa kambi ya upasuaji wa watu wanaolipia, wasiojiweza wanahudumiwa vipi?” alihoji.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku