Director Hanscana
Mtayarishaji wa video za muziki nchini, Hanscana amefunguka kwa kusema kuwa hakuna kilichopungua katika taaluma yake baada ya kuachana na kampuni ya ‘Wanene Entertainment’ ambayo alikuwa anafanya nayo kazi kwa muda mrefu.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Hanscana wamewataka wale wenye hofu na yeye juu ya kazi zake waangalie video ya wimbo ‘Inde’ ya Dully Sykes iliyotoka hivi karibuni.

“Hanscana ni Hanscana tu, hakuna kitu ambacho kitapungua au kimepungua, kama unataka kuthibitisha hilo angalia video ya Inde halafu njoo,” alisema Hanscana.

Aliongeza, “Mimi bado naendelea kujifunza, kila siku bado naendelea kujifunza, kwa hiyo mimi nataka mashabiki wangu waangalie hatua ambazo nazipiga. Soon studio yangu mpya itafunguliwa, sasa hivi nipo kwenye maswala ya usajili,”

Pia mtayarishaji huyo amesema kwa sasa anawasiliana vizuri na uongozi wa ‘Wanene Entertainment’ na hana tatizo nao.


Post a Comment

 
Top