Staa wa Nigeria, Wizkid, amethibitishwa kuwa atatumbuiza kwenye show ya Fiesta, Mwanza mwishoni mwa wiki hii.

Clouds FM wamethibitisha kumdondosha hitmaker huyo wa ‘Shabba’ Jumamosi, August 20.

“Kituuuuuuu #DealDone kwa mara ya kwanza ndani ya Mwanza #StarBoY wako @wizkidayo utatapata kumshuhudia LIVE juu ya jukwaa la #Fiesta2016 #Imooooo,” wameandika Clouds.

Hii itakuwa mara ya pili muimbaji huyo anakuja Tanzania. Mwezi October mwaka jana alitumbuiza kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.


Post a Comment

 
Top