Aug 15, 2016

Yanga Kukutana Kwa Dharura...Kisa Manji Kukusudia Kujiuzulu Baada ya Kutukanwa na Viongozi

Duru za taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinasema uongozi wa klabu hiyo kesho utakuwa na mkutano dharura kuelezea kuhusu taarifa za kujiuzulu kwa Mwenyekiti Yusuph Manji.

Kaimu Katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusderit, kupitia taarifa fupi aliyoituma kwa waandishi wa habari jioni hii amesema ni kweli mwenyekiti anakusudia kujiuzulu huku akitaja sababu kuwa ni kutukanwa,kudhalilishwa na kusakamwa na Mzee Ibrahim Akilimali na Paul Makonda huku kukiwa hakuna juhudi zozote za wanayanga kuchukua hatua.

Tamko hilo fupi lilimalizia kwa kusema "tumewasiliana na viongozi wa kanda na kesho tutakuwa na mkutano wa dharura utakaofanyika saa 4 kamili makao makuu ya klabu.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR