Aug 13, 2016

Yanga yavunja rekodi yao mbaya yaipiga waarabu 1-0


Yanga imeonyesha inaweza ila haikuamka mapema baada ya leo kulipa kisasi kwa kuichapa Mo Bejaia kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga imeitwanga Bejaia kwa bao la Thabani Kamusoko lililofungwa kwa kichwa kipindi cha kwanza akiunganisha krosi ya Juma Abdul.


Katika mechi ya kwanza kabisa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, Yanga ililala kwa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Bejaia.


Hii ni mechi ya kwanza Yanga imeshinda baada ya kucheza mechi tano, ikiwa imefungwa tatu, sare moja na kushinda moja ambayo ni ya leo.


Sasa Yanga ina pointi nne na inaendelea kubaki mkiani huku Bejaia inabaki na pointi tano sawa na Medeama ya Ghana huku TP Mazembe ya DR Congo ikiwa imejihakikishia kufuzu kwa kubaki kileleni na pointi 10.


Yanga ingeweza kupata mabao zaidi ya mawili lakini wachezaji wake wakapoteza nafasi nyingi za kufunga.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR