• Breaking News

  Aug 8, 2016

  Zitto Kabwe Atoa Neno Kuhusu Siku ya Wakulima..Adai Ilani ya ACT Wazalendo ilikuwa Bora zaidi Kuhusu Kilimo


  Leo ni siku ya Wakulima Tanzania. Chama chetu cha ACT Wazalendo kilikuwa na ilani bora zaidi kuhusu Kilimo kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 ( chanzo: Taarifa ya Waangalizi wa Uchaguzi na Muungano wa Wakulima MVIWATA ). Tujikumbushe ACT Wazalendo tulisema nini?

  Malengo

  Shabaha ya muda wa kati ni Kilimo kuingiza Fedha za kigeni USD 2bn ifikapo mwaka 2025.

  Shabaha ya muda mrefu ni kuuza nje Sukari na Mchele, kuongoza duniani kwa kuuza nje Katani na bidhaa za Katani, kuongoza Afrika kwa kuuza nje Korosho zilizokobolewa na Kila Mkulima wa Tanzania kuwa na Hihadhi ya Jamii

  Maagizo ya Kisera kwa Serikali

  1. Kufanya Kilimo kuwa shughuli Kiongozi katika kutokomeza umasikini nchini
  2. Kuanzisha Fao la Bei ( price stabilization ) na Bima ya Mazao na Mifugo katika Mfumo wa Hifadhi ya Jamii
  3. Kuendesha Kilimo kwa njia ya ' shamba kubwa katika mashamba madogo madogo ' ( integrated production schemes ) kwa kumilikisha wakulima Ardhi iliyobinafsishwa kwa wawekezaji na kuanzisha ' outgrowers scheme ' kuzunguka Mwekezaji mkubwa
  4. Kuweka Mfumo wa kodi unaoeleweka na usiotetereka ( stable agro fiscal regime )
  5. Kuanzisha Mamlaka ya Kilimo itakayosimamia Mazao yote, kuvunja bodi za Mazao na kuwa Msimamizi ( regulator ).
  6. Kuanzisha Soko la bidhaa ' commodities exchange ' na kuondoa kabisa watu wa Kati ( middlemen )
  7. Vyama vya Msingi vya Ushirika kuagiza wenyewe pembejeo moja Kwa moja kupitia Shirika la Umma maalumu Kwa ajili hiyo.

  Kura zetu hazikutosha kuunda Serikali. Serikali iliyochaguliwa inataka Viwanda kuwa Sekta Kiongozi katika kuondoa umasikini. Ushauri wetu kwa waliounda Serikali ni kwamba bila kuongeza uzalishaji na tija kwenye Kilimo sekta ya Viwanda haitakuwa na maana yeyote. Sekta Kilimo inapaswa kubakia kuwa sekta Kiongozi katika mapambano dhidi ya umasikini na sekta ya Viwanda na Kwa kuanzia Viwanda vya bidhaa za Kilimo kuwa ni kiungo muhimu. Mchumi Jorgenson anasema, ninanukuu kimombo ".... There must be a more balanced development of both the agricultural and industrial sectors without which overall economic growth would grind to a complete halt....."

  Ilani ya ACT Wazalendo 2015 inasema " ili kujenga uchumi shirikishi na kutengeneza Taifa linalofanya Kazi ( a working nation ) ni muhimu kufanya jitihada za makusudi katika kuhakikisha kwamba Kilimo kinaanza kuchangia vya kutosha katika ukuaji wa uchumi". Ikumbukwe kuwa mwaka 2015 Kilimo kilikua kwa kasi ya asilimia 3.3 tu ilhali sekta hii inapaswa kukua kwa wastani wa kati ya asilimia 8 - 10 Kwa muongo mmoja ili kuwezesha Nchi kutokomeza umasikini.

  - Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka nje licha ya mikwara kuku ya Serikali ya Awamu ya Tano
  - Tanzania bado ina Wakulima wa Mpunga ambao Mpunga wao unaoza ndani Kwa kukosa Soko Kwa sababu ya Mpunga kutoka Vietnam na Pakistan uliozagaa nchini
  - Tanzania inapata USD 700m tu Kama Fedha za kigeni kutoka mauzo ya bidhaa za Kilimo nje
  - Wakulima wameambiwa na Serikali wajitafutie pembejeo Serikali haina hela ya kuagiza
  - Wakulima wamezuiwa kuuza nje bidhaa zao wakati ndani hakuna Soko
  - Licha ya mikwara mbuzi, bado Ardhi imehodhiwa na wawekezaji wachache na Wakulima kukosa Ardhi ya kulima na kuendelea kukodishiwa
  - Juhudi za kuanzisha commodities exchange zimefia njiani na wachuuzi wanaendelea kuwanyonya Wakulima

  Wakulima amkeni.

  Zitto Kabwe
  Siku ya Wakulima 2016

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku