Aug 14, 2016

Zitto Kabwe Kaeleza Sababu za Kwa Nini Mohammed Dewji Apewe Asilimia 40 ya Hisa Simba SC

Najua headlines za vilabu vya Simba na Yanga kuombwa kukodishwa na Simba kununuliwa na bilionea wa 21 Afrika Mohammed Dewji ziligusa watu wengi na kila mmoja kutoa mawazo yake akiwemo mwanasiasa na mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe, Ayo TV ilimpata kwenye exclusive interview na kueleza kwa kina kwa nini alipendekeza Mohammed Dewji apewe asilimia 40 na sio 51 kama ambavyo anataka:
“Timu zetu hizi ni timu za watu kwa hiyo ni lazima mipango yoyote ya uboreshwaji wa timu isinyang’anye watu timu, hawa watu wamewekeza kwa muda mrefu katika timu zetu hizi zenye miaka zaidi ya 70, kwa mfano MO anatakiwa kupewa sio zaidi ya asilimia 40 ili akitaka kufanya maamuzi ashirikishe wanahisa wengine na sio kumpa 51 awe anafanya maamuzi peke yake”Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA

Post a Comment

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © Siasa Huru l Habari za Siasa | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by SiasaHuru.com