• Breaking News

  Sep 17, 2016

  APIGWA Risasi Akijaribu Kuwatoroka Mikononi Mwa Polisi

  Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi mguuni na polisi wakati akijaribu kuwatoroka.

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo ni kati ya  watano waliokamatwa kwa tuhuma za  kuvamia maduka makubwa na kupora mali jijini Dar es Salaam.

  Sirro alisema tukio hilo lilitokea Septemba 14 eneo la Ununio wakati mtuhumiwa akiwapeleka polisi kuwaonyesha ilipokuwa imefichwa silaha  kwenye majaruba ya chumvi.

  Alisema mtuhumiwa alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali kwa matibabu kutokana na kutokwa damu nyingi.

  Awali, alisema watuhumiwa hao, akiwamo mwanamke, walikamatwa katika eneo la Goba na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na matukio hayo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku