• Breaking News

  Sep 8, 2016

  Asafirisha Dawa za Kulevya Kwa Njia ya Posta

  Raia wa Kenya mwenye asili ya Uingereza, Christopher James na mfanyakazi wake, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine zenye uzito wa gramu 7.5 kwa njia ya posta.

  James, mmiliki wa kampuni ya Walter Dividing Sport alikamatwa jana na kikosi cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar, akituhumiwa kusafirisha dawa hizo kutoka Unguja kwa sanduku la posta  eneo la Kijangwani, Kaskazini Unguja.

  Mkuu wa kikosi hicho, Kamishna Juma Amir Juma amesema  mtuhumiwa huyo alishirikiana na mfanyakazi wake, Nassoro Othmani Ally (43), mkazi wa Mtipula kusafirisha dawa hizo.

  “James alikamatwa katika kitongoji cha Kijangwani akiwa na bahasha aliyokuwa akiituma kwa njia ya posta kupeleka nchini Australia,” amesema.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku