• Breaking News

  Sep 8, 2016

  Raia wa China Afariki Akipanda Mlima Kilimanjaro

  Moshi. Raia mmoja kutoka nchini china aliyefahamika kwa jina la Zhuu Yush(27) amefariki dunia wakati akipanda Mlima Kilimanjaro kutokana na matatizo yaliodaiwa kuwa ni hali ya hewa iliyoko eneo la mlimani.

  Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa amesema umauti ulimkuta raia huyo  jana  saa saba mchana maeneo ya Jiwe la Kamba tarafa ya Kibosho Ubwe wilayani Moshi.

  Mutafungwa alisema kuwa raia huyo aliingia nchini Agosti 3 mwaka huu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa(KIA) ambapo alikutwa na baadhi ya vitambulisho na paspoti ya kusafiria yenye namba E43941606.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku