• Breaking News

  Sep 5, 2016

  CUF: Tutaendelea Kuitafuta Haki Kwa njia ya Demokrasia

  Mtatiro
  Chama cha wananchi CUF kimesema kitaendelea kusimamia kuimarishwa kwa demokrasia nchini hususan visiwani Zanzibar kwa njia ya amani, licha ya matamko mbalimbali yanayotolewa na baadhi ya viongozi kukibeza chama hicho katika harakati zake za kutafuta maelewano kwa amani na kwa njia ya demokrasia.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amesema CUF itaendelea kuitafuta haki kwa njia ya kidemokrasia.

  “Sisi kama chama tunajua demokrasia ya nchi inapita katika wakati mgumu,lakini sisi kama chama cha siasa ambacho kipo kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, tutazidi kuungana na Watanzania, kuwaongoza watanzania, kuungana na wazalendo na watu wote wanaolipenda taifa hili,” alisema Mtatiro.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku