Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ ambaye haishi vimbwanga, Alhamisi hii amefunguka kwa kudai kuwa hamjui msanii, Ruby ambaye aliwai kufanya vizuri na wimbo ‘Na Yule’.

Aidha amedai pia hamjui video queen Giggy Money ambaye hivi karibuni ameonekana kwenye video ya ‘Inde’.

Akiongea katika kipindi cha Papaso cha TBC FM Alhamisi hii, Diva aliulizwa endapo akikutana na Ruby ambaye ameachana uongozi wake wa zamani atamshauri nini, ndipo mtangazaji huyo alipojibu kwamba hamjui msanii huyo.

“How is Ruby? Simjui na sijawai kumsikia,” alisema Diva.

Hata hivyo, Diva hakueleza nini kilitokea kati yake na msanii huyo ambaye aliibuliwa na Serengeti Super Diva 2014 na baadae kupewa msaada zaidi na THT pamoja na Clouds FM.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya SIASA HURU Kwenye Simu yako ili Kupata Habari zetu Haraka


POST A COMMENT

Post a Comment

 
Top