• Breaking News

  Sep 29, 2016

  DONALD Trump Akasirishwa na Wasaidizi Wake Kukiri Kuwa Alibwagwa na Clinton Kwenye Mdahalo wa Kwanza

  Donald Trump anaamini kuwa alifanya vizuri kwenye mdahalo wa kwanza dhidi ya Hillary Clinton – lakini kura zinasema tofauti, hata wasaidizi wake pia wanaamini kuwa alikula za uso!

  Clinton, Trump pick up big wins

  Kinampa hasira kuona kuwa wasaidizi na washauri wake wanakubali maneno ya vyombo vya habari kuwa hakufanya vyema kwenye mdahalo huo, kwa mujibu wa CNN.

  Wasaidizi wake walimshauri abadilishe namna anavyojiandaa kwenye mdahalo ujao lakini hataki kusikia lolote.

  Trump anataka wafuasi wake wamtetee kwa anachokifanya na amekataa kukubali kuwa alifanya vibaya licha ya kura kuonesha kuwa Clinton alipata asilimia zaidi ya 60 huku yeye akicheza kwenye 27 tu.

  Wagombea hao wa Urais wa Marekani watakutana kwenye mdahalo wa pili October 9.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku