• Breaking News

  Sep 28, 2016

  DRAMA: Mama Diamond ampongeza Wema kwenye birthday yake baada ya kumkaushia Zari

  Mama Diamond, Bi Sandra, amemtonesha mchumba wa mwanae, Zari pale panapomuuma zaidi.

  Amempongeza ex wa Diamond, Wema Sepetu katika birthday yake, Jumatano hii, Septemba 28, siku chache tu baada ya kumkaushia Zari kwenye birthday yake – ajabu!

  Happy birthday.. Mamy akee @wemasepetu mungu akuongezee umri na akujali kheri akufungulie Mlango wa baraka kwa kila uliombalo.Amin๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜ ๐Ÿ‘‘๐ŸŽ‰๐ŸŽŠ,” ameandika Bi. Kendrah Jumatano hii.

  Post hiyo inadhihirisha uvumi wa muda mrefu kuwa Zari haelewani na mama mkwe wake huyo pamoja na ndugeze wengine wake Diamond. Wifi yake, Esma naye alimkaushia raia huyo wa Uganda mwenye makazi yake Afrika Kusini.

  Kwa muda sasa Zari na mama mkwe wake hawana maelewano mazuri

  Minong’ono inadai kuwa Zari hakubaliki ukweni kutokana na kupenda maisha ya kizungu, kutawala mipango ya Diamond na huenda ndio chanzo cha Bi Sandra kuondoka Madale, nyumbani kwa staa huyo.

  Pamoja na Zari kutokubalika ukweli, Diamond haoneshi kushtushwa na hali hiyo kwakuwa hivi karibuni alimzawadia nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 396 ya Afrika Kusini pamoja na kumpeleka visiwani Zanzibar kusherehekea birthday yake.

  Labda ndugu za Diamond inabidi waukubali tu ukweli mchungu kuwa Zari sasa ndio kila kitu kwa staa huyo. Wakiwa na mtoto mmoja sasa, Tiffah, wawili hao wanatarajia kuongeza mtoto wa pili December mwaka huu

  1 comment:

  1. VIMAMA VINGINE VINAKUWAGA VICHAWI TU,KIMTAZAMO TU UTAMUONA ..ZARINA KAMPAISHA DAI ANOTHER LEVEL .YY ALITAKA AWE UNDER GROUND NA BISHOW WEMA WATU WANAANGALIA MBALI.ONASASA UTAJIRI ALOKUWANAO DAI NI JUHUDI NA ZA ZARI SIO HUYO AU HAO WANAWAKE ZAKE WA KILA SIKU SHEREHE.KILA MTU ANAPESA HAPO HAKUNA TEGEMEZI HAPO.SASA MAKUWA INTERNATINAL ZAID NANI ZARI AMECHANGIA.KWANZA ILE DADAKICHWA MCHAGA KAZINGIZIWA UNIVERSITIES UKWELI USEMWE HACHENI UNAFIKI..GOOO DAI GOOO ZARINA HASSAN...WISH U ALL THE BEST..

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku