• Breaking News

  Sep 3, 2016

  Elizabeth Asenga Afikishwa Mahakama ya Kisutu kwa Kumuita Rais ''Kila.za'' na ''Fala''

  Elizabeth Asenga (40) amefikishwa kortini  katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kumuita Rais Magufuli "******".

  Akisoma mashtaka hayo Leonard Chalu wakili wa serikali mbele ya Huruma Shahidi alidai kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kosa la matumizi mabaya ya mtandao.

  Mtuhumiwa aliandika kwenye mtandao wa whatsup kuwa "Good morning humu, nakuja Rais ****** kama huyo wetu, angalia anampa Lissu umashuhuri fara lile,picha yake ukiweka ofisini nuksi tupu, ukiamka asubuhi ukikutana na picha yake kwanza siku hiyo inakuwa na mkosi mwanzo mwisho"

  Mshitakiwa amekana mashtaka yake amepewa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili kila mmoja asaini hati ya shilingi milioni 3.

  Shauri hilo litatajwa tena tarehe 22.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku