• Breaking News

  Sep 3, 2016

  FREEMAN Mbowe Azungumzia Kuhusu Shirika la Nyumba NHC Kutoa Mali zake nje

  Freeman Mbowe
  Shirika La Nyumba la Taifa kupitia kampuni ya udalali juzi zilitoa samani mbalimbali katika jengo la Club Bilicanas na jengo lenye Ofisi ya Free Media kufuatia mmiliki wa ofisi hizo Freeman Mbowe kutolipa deni ambalo ilielezwa kuwa anadaiwa naa shirika hilo.

  Kufuatia hatua hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa sio kweli kwamba shirika hilo linamdai fedha kwa sababu amekuwa akitumia majengo hayo kwa takribani miongo miwili sasa na mara zote amekuwa akilipa kodi kwa wakati.

  Shirika la Nyumba la Taifa mwezi uliopita lilitoa taarifa kuwa Mbowe na baadhi ya wateja wengine ni wadaiwa sugu kwa sababu hawajalipa malimbikizo ya kodi wanazodaiwa na hivyo kupewa notisi kuwa hadi tarehe 31, Agosti 2016 wawe wamelipa la si hivyo, wataondolewa katika majengo hayo.

  Mbowe amesema kinachofanyika hapa ni siasa kwani wanafanya kama kumkomoa kwa sababu mara zote amekuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali kuhusu hali ya siasa nchini.

  Aidha amesema kuwa, kama ni kweli shirika hilo lina nia ya dhati ya kukusa kodi, je! Ni watu wangapi wanadaiwa? kama wapo wengine kwanini hadi sasa ni samani zangu tu zimetolewa.

  Shirika la Nyumba la Taifa lilitaja pia taasisi za serikali ambazo nazo zinadaiwa kodi ambazo ni pamoja na;

  Ofisi ya Rais inadaiwa zaidi ya Sh milioni 10.
  Wizara ya Uchukuzi inadaiwa zaidi ya Sh bilioni 2.
  Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi  yenye deni la Sh bilioni 2,
  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inayodaiwa zaidi ya Sh bilioni moja,
  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inadaiwa zaidi ya Sh bilioni moja,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, inadaiwa Sh milioni 613,
  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inadaiwa Sh milioni 360.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku