• Breaking News

  Sep 27, 2016

  HESHIMA kwa Wanaume Wanaotimiza Majukumu yao

  Habari wanajamvi, poleni kwa shughuli za ujenzi wa familia na taifa kwa ujumla.

  Narudia tena heshima kwao WANAUME.
  hawa ni wale ambao wanatambua nafasi zao kama MWANAUME.

  Nimekuwa nikiwaza, kama ningekuwa mwanaume,je ningeweza kufanya hayo wafanyayo? Hivi inakuja naturaly au inakuwaje!!

  Mwanaume ni mpenzi wako, anakujali, anakusikiliza,unakuhudumia, anakuthamini na kukulinda.
  Wote mnafanya kazi na inawezekana unamzidi kipato, lakini bado anakuhudumia kwa shida zako as if yeye hana zake. Akikwama yeye atahangaika hata kukopa kwa washkaji mambo yaende sawa.

  Bado ukiwa na tatizo la kuhitaji ushauri, atakushauri kwa upendo, atakuvumilia na maswali yako ya kipuuzi puuzi, anakuelekeza kwa upendo.

  Ni baba wa familia,anahangaika na kazi nyingi za kuhakikisha familia inasimama, ni MUME kwa mkewe na BABA kwa wanawe. Anahangaika na familia yake,ya mkewe na ndugu wengine pia.

  MWANAUME hata akiwa rafiki yako wa kawaida tu, anakuwa rafiki mzuri sana.

  Kwakweli mie mwanaume wa hivi namuheshimu na kumtii kupita maelezo,na kuchunga sana nisimkosee hata nikimkosea na kugundua nimemkosea basi nitajishusha na kumuomba msamaha wa dhati na kujichunga nisirudie kosa.

  Heshima kwenu WANAUME, kwakweli mnatufaa na kuturahisishia maisha.

  Hii haiwahusi wale waliogoma kuwa WANAUME.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku