• Breaking News

  Sep 5, 2016

  Hoteli ya kifahari ya Arusha ‘Snow Crest’ kupigwa mnada, ni kutokana na kutolipa michango ya NSSF

  Hoteli ya Kifahari ya Arusha iitwayo Snow Crest itapigwa mnada mwezi huu kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye gazeti.

  Tangazo hilo lililotolewa na kampuni inayojulikana kama First World Investment Court Brokers, limedai kuwa hoteli hiyo itapigwa mnada Septemba 23, saa tano asubuhi.

  Mwakilishi wa kampuni hiyo, Allan R Mollel ameiambia Bongo5 kuwa hoteli hiyo ilipelekwa mahakamani na shirika la hifadhi ya jamii, NSSF kwa kushindwa kuwalipa wafanyakazi michango yao.

  “Hiyo hoteli inauzwa kwasababu ya kesi iliyokuwa mahakamani ambayo hoteli hiyo inadaiwa na NSSF michango ile ya wafanyakazi kwa maana kwamba hiyo hoteli walikuwa hawafikishi michango ya wafanyakazi NSSF. Kwahiyo NSSF wakafungua kesi wameshinda na wakaomba kuuza hii hoteli ili kuweza kupata michango hiyo ya wafanyakazi,” Mollel ameiambia Bongo5.

  Amedai kuwa NSSF inaidai hoteli hiyo shilingi milioni 442 ambazo ni michango ya NSSF kwa wafanyakazi wake. Hata hivyo Mollel amesema kisheria hoteli hiyo bado ina nafasi ya kuzilipa fedha hizo kwa NSSF pamoja na gharama za dalali na wakaendelea kuwa na umiliki wa hoteli hiyo.

  “Sasa hivi kilichoongezeka hapo ni gharama za dalali,” amesema.

  “Kama wataweza kulipa fedha zote wanazodaiwa na NSSF, wakalipa na gharama za dalali, mambo yatakuwa yamefika mwisho.”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku