• Breaking News

  Sep 9, 2016

  Inashangaza: Mwanafunzi wa Miaka 13 Ajifungua Shuleni

  Msichana wa shule ya msingi aliwashtua waalimu na wanafunzi wengine baada ya kujifungua akiwa shuleni

  Mwanafunzi huyo wa miaka 13 hakuwa na dalili za ujauzito. Alijifungua katika makao ya shule bila usaidizi na kusemekana kupata majeraha.Msichana wa shule ya msingi aliwashtua waalimu na wanafunzi wengine baada ya kujifungua akiwa shuleni

  Wanafunzi na walimu walishangaa hasa kutokana na kuwa mwanafunzi huyo hakuonekana kuwa mjamzito.

  Mwanafunzi huyo wa umri mdogo aliumia baada ya kujifungua peke yake. Alipelekwa katika hospitali ya wilaya ya Naivasha punde baada ya walimu kugundua kilichokuwa kimeendelea.

  Mwanawe alifariki baada ya masaa kumi na mawili.

  “Kulikuwa na hatari kubwa ambapo alijeruhiwa wakati wa kujifungua, alipata matatizo mengine pia alipokuwa akijifungua,” alisema daktari.

  Madaktari walisema mtoto alifariki kutokana na matatizo ya kupumua.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku