• Breaking News

  Sep 11, 2016

  Kampuni ya Fast Jet Kupunguza Wafanyakazi

  Kampuni  binafsi ya usafiri wa anga, Fast Jet imeamua kupunguza wafanyakazi ili kwenda sambamba na gharama za uendeshaji.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Fast Jet, John Corse ametoa taarifa kwa gazeti la The Citizen inayoeleza kuwa watapunguza wafanyakazi kutokana na mabadiliko ya kimuundo na uendeshaji.


  “Wateja wamepungua, hawapandi ndege sasa. Hivyo ili kampuni ipate faida, ni lazima ipunguze baadhi ya wafanyakazi ili kuendana na gharama za uendeshaji,” anasema Corse kwenye taarifa hiyo.


  Alipoulizwa kama sababu ya kupunguza wafanyakazi inaweza kuwa inatokana na mikakati ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Corse amejibu: “Si kwa sababu ATCL inafufuliwa bali ni changamoto za kibiashara.”


  Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alitangaza kuwa ndege mbili ambazo Serikali iliahidi kuzinunua zitafika nchini kati ya Septemba 19 na 25.  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku