• Breaking News

  Sep 6, 2016

  Katibu Mkuu wa UN, Kofi Annan Azomewa Nchini Myanmar

  Wanaharakati wa Kibudha nchini Myanmar wamemzomea na kumkemea Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan.

  Bw Annan alizomewa baada ya kuwasili katika jimbo la Rakhine kuchunguza mzozo wa kidini katika eneo hilo.

  Maelfu ya Waislamu wa jamii ya Rohingya wametimuliwa kwenye makao yao baada mashambulizi yaliyotekelezwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni Wabudha, huku wengi wao wakinyimwa uraia na kulazimika kuikimbia nchi hiyo.

  Mashambulio hayo yamepelekea baadhi ya watu kutilia shaka kujitolea kwa kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi kutetea haki za kibinadamu.

  Bi Suu Kyi alimwita Bw Annan kuchunguza na kupendekeza njia za kupunguza uhasama baina ya jamii zinazoishi eneo hilo.

  Bw Annan alihusika kupatanisha pande hasimu wakati wa vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku