• Breaking News

  Sep 23, 2016

  KOREA Kusini Yapanga Kumuua Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un

  Korea Kusini imejipanga kumuondoa duniani kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un iwapo itahisi kutishwa na shambulio la silaha kinyuklia, waziri wa ulinzi wa nchi hiyo amesema, CNN imeripoti.

  Alipoulizwa bungeni kama kuna jeshi maalum lililo tayari kumuua Kim Jong Un, Han Min-koo alisema: “Ndio, tuna mpango huo.” “Korea Kusini ina mpango wa jumla kutumia silaha nzito kulenga miundo mbinu ya adui katika maeneo makubwa pamoja na kuuondoa uongozi wa adui,” aliongeza.

  Kwa muda sasa kulikuwepo na tetesi za kuwepo mpango huo lakini jibu hilo la wazi la waziri huyo limewashtua wengi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku