• Breaking News

  Sep 5, 2016

  Kujenga Barabara Kwa Viwango Duni Kisha Kunafanyiwa Ukarabati Kila Mara ni Kuchezea Kodi zetu

  Boresheni miundo mbinu ya barabara. Mnashangaza sana mnapofanyia matengenezo barabara ambazo zimeshawekwa lami alafu mnaleta maskaveta yenu mnakwangua hiyo lami baada ya miezi minne tu, huu ni uharibifu na utumiaji wa kodi zetu bila huruma.

  Mfano halisi ni hii barabara ya Kilwa tangu Magufuli awe waziri na mpaka amekuwa Rais hii barabara imebanduliwa lami hii ni mara ya tano sasa ukipita leo utakuta migari imeziba njia kisa wanabandua lami wanaweka mpya, what 4?

  Njia ya Pugu nayo ni hivyo hivyo ukipita sasa hivi ile lea ya kujazia tayari imevuka kama si kufikia mwisho wa kujazia lami. Ni matumizi mabaya ya kodi zetu.

  Kuna mitaa mingapi haijui njia ya kokoto wala kuwekewa lami miaka nenda miaka rudi. Mnajifanya hamuoni haya.

  Kutwa kuzungukia mitaa ya wakubwa wenu kuangalia kama taa ya barabarani imeungua ili mbadilishe wapi kuna shimo hata la kupenya panya mnaleta greda mnachimba mnamwaga kokoto mnaweka lami mnapiga chenu cha juu.

  Ushauri:

  Kuweni wabunifu katika kutengeza mazingira mapya ya jiji na nchi kwa ujumla. Ingieni kwenye mitaa kagueni njia zote za mitaa. Mbagala tu ni wapi kuna mtaa ambao umewekewa lami lakini utaona mijitu inakazania kubandua lami barabara ya Kilwa kila baada ya miezi kadhaa mitaani wanakula vumbi tu alafu mnasema mna wataalamu mainjinia wa ujenzi wa miuno mbinu kumbe hamna kitu ni wapiga dili tu.

  Kaeni vikao na serikali za mitaa fanyeni utaratibu wa kuhamisha watu mpate njia mpya za mitaa ili mjenge pia kwa kiwango cha lami hii ndio mikakati tegemeo kwa maendeleo ya jamii yetu.

  Msiishie kubandua lami tu wakati mitaani wananchi walipa kodi wanlishwa vumbi tu kila mwaka.

  Aibu!!

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku