• Breaking News

  Sep 7, 2016

  Kutoka Bungeni: Fao la Kujitoa Halipo Badala yake Limeletwa fao la Kutokua na Ajira

  Kutoka bungeni Dodoma

  Mswada wa mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii uko tayari. Fao la kujitoa halipo kwenye mapendekezo hayo, badala yake limeletwa fao la kutokua na ajira

  Inapendekezwa kuwa, mfanyakazi ambaye amechangia zaidi ya miezi 18 atalipwa 30% ya mshahara wake wa mwisho baada ya kupoteza ajira. Na atalipwa kwa miezi 6 mfululuzo, baaada ya hapo malipo hayo yatasitishwa.

  Mfanyakazi anayestahili malipo haya, ni yule tu ambaye hakuacha kazi kwa hiari yake (resignation)

  Baada ya miaka 3 tangu kusitishwa kwa fao la kujitoa, mfanyakazi atakayekuwa hajapata ajira ataruhusiwa kuhamisha michango yake kutoka kwenye mfuko wa lazima (compulsory scheme), kwenda mfuko wa hiari (supplementary scheme). Hapo ataruhusiwa kuchukua 50% ya michango yake.

  Hapa ndio wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi tunatakiwa tuunganishe nguvu kutetea maslahi ya wafanyakazi ambao hawana ajira za kudumu.

  4 comments:

  1. Sijui kama waliopo madarakani yaani wote wanaohusika na hili la mifuko ya jamii wapo kwa ajili ya kutetea maisha ya mnyonge hasa mwenye kipato cha chini au ni kwa manufaa ya serikali. Kwa hiyari ama kulazimishwa mwananchi huyu anakubali kujiunga na kuchangia mfuko fulani wa jamii.Hatimaye hana mamlaka ya kuichukua pesa hiyo atakapoihitaji na kama ataichukua ni kwa mashariti hayo magumu waliyoyaweka. Mimi naamini wananchi wanaweza kuhifaddhi fedha zao na si katika mifuko ya jamii. Tchao

   ReplyDelete
  2. Enter your comment...SIO HALALI NI UONEVU.

   ReplyDelete
  3. serikali wanatakiwa kuwajali wanachi kwa kuruhusu wafanya kazi kuchukua fedha zao bila sheria kwani wakati wa kujiunga na hifadhi husika ilikuwa ni hiari siyo shuruti na inapofika wakati wa kutoa in kuwa masharti magumu, fedha hizo ni haki ya mfanya kazi na haina hata nyongezo yoyote. Mimi nashauri bunge letu liangalia muswada huu kwa jicho la pili na siyo kwa kuangalia viongozi wakubwa wa nchi hii kwani wao wanakula bila jasho ukilinganisha na wanyonge wenye maisha ya chini.

   ReplyDelete
  4. serikali wanatakiwa kuwajali wanachi kwa kuruhusu wafanya kazi kuchukua fedha zao bila sheria kwani wakati wa kujiunga na hifadhi husika ilikuwa ni hiari siyo shuruti na inapofika wakati wa kutoa in kuwa masharti magumu, fedha hizo ni haki ya mfanya kazi na haina hata nyongezo yoyote. Mimi nashauri bunge letu liangalia muswada huu kwa jicho la pili na siyo kwa kuangalia viongozi wakubwa wa nchi hii kwani wao wanakula bila jasho ukilinganisha na wanyonge wenye maisha ya chini.

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku