• Breaking News

  Sep 16, 2016

  Kutokuonekana kwa Magufuli Toka Tetemeko, Kunatetemesha!

  Na. M. M. Mwanakijiji

  Inawezekana kabisa zipo sababu kubwa na za msingi kabisa za kwanini Rais Magufuli, Rais wa wanyonge na mtetezi wa maskini hajaonekana kuzungumza na taifa na sehemu kubwa ya nchi ambayo imekuwa kwenye mshtuko kufuatia tetemeko la ardhi lililopiga Kagera na kurindima sehemu kubwa ya Kaskazini Magharibi mwa nchi yetu Jumamosi iliyopita. Sababu hizi zinaweza kuwa ni za msingi kabisa na zenye maana endapo zitatolewa na watu wote wenye fikra huru wakaweza kukubaliana nazo.

  Kuna sababu hata hivyo ambazo zikitolewa – kama zitatolewa – zitawafanya watu waangaliane mara mbilimbili kama wanaozitoa hizo sababu wanazitoa wakifikiria watu wote hawana uwezo wa kufikiri au wanajaribu kulazimisha wasifikiri.

  Baadhi ya sababu ambazo haziwezi kutolewa na kwa kweli hazipaswi kutolewa ni kama “hili ni suala la viongozi wa chini, siyo suala la Rais” au “mbona Waziri Mkuu alishaenda na suala la maafa liko chini ya Waziri Mkuu”. Sababu nyingine ambazo hazipaswi kutolewa au hata kujaribiwa kutolewa ni kama kuamua kusema “lilikuwa janga la kawaida tu hawakufa watu wengi”. Wenye kutoa sababu hiyo wanaweza wakasema kuwa ili Rais aonekane na kuzungumzia na kwenda kutoa mahali pole basi janga linapaswa kuwa kubwa sana na lenye vifo vingi sana; kwamba vifo 16 kwenye tukio hili sivyo vya kusitusha sana kwani Watanzania tayari wameshazoea kupata habari za ajali zenye kuua watu wengi.

  Wenye kutoa sababu hii wanaweza kuendelea na kusema kuwa tayari ajali za magari zinaua watu wengi sana na siyo mar azote au hata mara moja Rais hajaenda kutembelea maeneo ya ajali. Kwamba, kuna ajali zimeua watu thelathini au ishirini lakini Rais anaishia kutoa pole na rambirambi tu.

  Tatizo la sababu hii ni kuwa suala la tetemeko la ardhi ni zaidi ya ajali; ni mojawapo ya matukio makubwa ya nguvu za asili za ulimwengu (natural occurring event) ambayo mwanadamu hajaweza kuyapatia majibu ya kutosha kujiandaa nayo. Kwa maneno mengine, tukio la tetemeko la ardhi siyo “ajali” kwa maana ya ajali bali ni “baa” ni “janga”. Matukio mengine yanatokana na nguvu hizi za asili za ulimwengu ni kimbunga, mafuriko, moto, n.k

  Hivyo, kuchukulia janga la tetemeko la ardhi kama ni ajali tu mojawapo ni kutokuwa makini na kutoonesha kujua uzito wa tukio hili. Tetemeko hilo lingepiga hadi kufikiria hata kiasi cha alama namba 7 kwenye kipimo cha Richter basi hadi Mwanza, Mara na inawezekana hata Kigoma kungesikika kilio kama siyo mpaka Dodoma! Hivyo, mshtuko wa tukio hili peke yake kwa eneo kubwa la nchi yetu na lenye watu wengi ingemlazimu Rais mwenyewe kuhakikisha anajitokeza mara moja kuwatuliza wananchi na kuwapa moyo watu waliokuwa kwenye juhudi za kufanya uokoaji.

  Lakini pia kuna sababu nyingine ambazo hata zikitolewa bado watu wataona zina shida. Kwa mfano, ni vigumu kuwafanya watu waamini kuwa Rais alikuwa ‘busy’ sana na mambo mengine ya kitaifa – kama kufanya teuzi mbalimbali na kuwaapisha watu mbalimbali – kiasikwamba hakuwa na muda way eye mwenyewe kujionesha kuwa anajali kilichowatokea watu wake. Hivi, watoto wa Kitanzania wanapolala nje, wananchi kukosa makazi ya kudumu, watoto (kwa maelfu) kuwa katika hali ya mshtuko wasijue wazazi wao watafanya nini kuwahakikisha malazi, makazi na vyakula siyo sababu ya Rais mwenyewe kujionesha na kuwatuliza moyo wananchi hawa na familia zao? Siwezi kuona ubusy wowote ule ambao unaweza ukawa sababu au kisingizio cha kwanini Rais hajatokea kuzungumza na taifa na kutembelea Bukoba.

  Ni MAKALA NDEFU - kwa wanaoependa kuendelea kusoma Bonyeza HAPA

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku