• Breaking News

  Sep 25, 2016

  LWAKATARE Akabidhi Mifuko 400 ya Saruji Aliyoahidi Edward Lowassa

  Meya wa Manispaa ya Bukoba, Adronikus Karumuna amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu mifuko 400 ya saruji iliyoahidiwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi.

  Akikabidhi msaada huo leo, Karumuna amesema kuwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Lowassa jana kutokana na uamuzi wa Chadema.

  Tukio hilo limeshuhudiwa na Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare ambaye amesema kwa sasa wananchi wanahitaji msaada na hivyo hakuna sababu ya kuwa na malumbano kwa sababu yoyote.

  Jenerali Kijuu ameueleza ujumbe huo kuwa anatumikia wananchi wote kwa usawa bila kuangalia misimamo yao ya vyama na kutoa wito wa wadau wengine kujitokeza kutoa misaada zaidi.

  Mwananchi

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku