• Breaking News

  Sep 16, 2016

  Mahakama Yatupilia Mbali Mapingamizi Manne ya NHC Dhidi ya Mbowe


  Mahakama kuu kitengo cha ardhi imetupilia mbali mapingamizi manne ya kisheria yaliyowekwa na mawakili wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) likiongozwa na wakili Sekule.

  Mahakama imeshawishika na hoja zilizojibiwa na jopo la mawakili likiongozwa na Peter Kibatala Kuwa hoja hizo hazina mashiko kisheria.

  Judge wa Mahakama Kuu ameshawishika na kesi mbalimbali ambazo zimetumiwa kushawishi mahakama isizitilie maanani MAPINGAMIZI Hayo.

  Imesema vifungu ni sahihi na njia iliyotumiwa na mawakili wakiongozwa na KIBATALA ni sahihi.

  Pia Kuhusu Mkataba imesema hilo suala linabishaniwa na linahitaji ushahidi na Mahakama haiwezi kulichukulia juu kama NHC wanavyotaka

  TENA Kuhusu madai ya NHC kuwa Mkataba wa umiliki wa pamoja(JOINT VENTURE) wa Jengo kati yake na Mbowe kumalizika 2015; mahakama imesema hilo suala linabishaniwa na linahitaji ushahidi na Mahakama haiwezi kulichukulia juu kama NHC wanavyotaka

  Judge amesema ameshindwa kushawishika na hoja na hata sheria ambazo mawakili wa shirika la nyumba wamezitumia.

  Kesi hiyo itaendele tarehe 27/9/2016 katika mahakama hiyo kwa kusikiliza maombi ambayo Mawakili wanomuwakilisha Mbowe Hotels Ltd ambayo mojawapo ni kurudisha vitu ambavyo NHC na Dalali wamevitoa sehemu yenye mgogoro kama ambavyo vilikutwa!.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku