Sep 2, 2016

Makonda: Oktoba Mosi ni siku Maalum ya Upandaji Miti Dar

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwa mfano wa kuigwa katika kutunza mazingira ambapo amesema siku ya Oktoba Mosi itakuwa siku maalumu ya upandaji miti Dar es Salaam.

Ameyasema hayo Ahamisi hii katika maadhimisho ya miaka 52 jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) eneo la Lugalo ambapo alishiriki usafi na viongozi wa dini mbalimbali katika eneo la jeshi Lugalo.

“Kwahiyo tarehe moja ni tarehe ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, jeshi la wananchi, polisi, wahamiaji, magereza,JKT, vitakuwa pamoja nasi na viongozi wetu wa dini tumekaa vikao jana tumeongea, namna gani ambavyo watatusaidia katika makanisa na misikiti kuhakikisha tunapanda miti mingi katika mkoa wetu wa Dar es Salaam, “alisema Makonda.

Aidha Makonda alitoa wito kwa vyombo vya usalama ambavyo vipo kando ya barabara kuhakikisha kuwa vinakuwa mfano katika uboreshaji wa mazingira katika eneo husika.

“Mmefanya kazi kubwa sana naomba niwapongeze, kwa barabara yetu hii ya kutoka Kawe mpaka Mwenge barabara ambayo imekuwa ni mfano na nimeshamuagiza Kamishna Sirro, nataka kuona upande wao kule nako barabara yao inakuwa mfano. Sehemu yoyote ambapo kuna kambi ya Jeshi lakini mbele yao kuna barabara lazima barabara zifanane kama vile mlivyofanya wanajeshi katika barabara kutoka Kawe mpaka Mwenge,” alisema Makonda.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR