• Breaking News

  Sep 16, 2016

  MALEZI: Nilichokiona kwenye gari la shule la watoto wetu

  Wazazi wenzangu hili linawahusu sana. 

  Naomba kila mmoja mwenye mtoto anayesoma azingatie na kulitilia uzito kwa kufanya ufwatiliaji wa kina. Iko hivi, jana wakati natoka kutekeleza majukumu yangu, nikiwa barabarani nilipishana na gari la shule. Jina la shule na namba ya gari navihifadhi. Ndani yake lilikuwa na watoto wa jinsia zote. Maana nilipiga jicho kwa haraka kwakuwa nilikuwa speed kwenye highway.

  Hakika nilistushwa na nilichokiona. Siti ya tatu kutoka nyuma niliona watoto wawili wakiume wakiwa wanafanya "deep kissing" . Walikuwa wanafanya romance. Niliogopa na kushtushwa sana huku nikitamani kumwambia dereva asimame na kuwakanya hao watoto. Sikuweza maana highway tuliyopo ilikuwa busy sana. Niliendelea na safari yangu kwa masikitiko makubwa sana.

  Nilitafakari hali ya sasa ya vijana wetu wengi wakijihusisha na vitendo vya ushoga. Safari yao ya ushoga ama u lesbian huanzia huku. Huanzia huku kwenye magari ya shule ambapo matron anakaa kiti cha mbele na dereva wakiwaacha watoto wakiiga yale wanayoyaona kwenye TV. Nilishtushwa kuona watoto wetu wakiyatenda haya huku tukiamini watoto wetu wapo salama.

  OMBI:
  Wazazi fuatilieni kama magari ya shule yana muangalizi/patron/matron wa watoto wenu. Na mhoji namna matrons wanavyo angalia watoto wakati wa kuwarudisha na kuwachukua majumbani.

  Pia kama mtoto wako ni wa mwisho kushushwa au wa kwanza kuchukuliwa amini ipo hatari juu yake. Madereva wa watoto wetu wapo ambao sio waaminifu. Huwafanya vibaya watoto wa mwisho kuwashusha na hata wale wa kwanza kupanda.

  Ongeeni na watoto juu ya shule wanazosoma. Kulipa ada kubwa hakutamsaidia mtoto kama hakuna ufwatiliaji. Mtoto anaweza akawa na maendeleo mazuri darasani na ukaridhika kabisa yupo shule nzuri. Maendeleo yakakutia motisha kutafuta ada. Lakini mali bila daftari hupotea bila habari. Elimu bila ufuatiliaji ni kazi bure.

  Ushoga au u lesbian hauji kama ajali. Huwa na mwanzo wake. Tunaweza kuwaokoa watoto wetu kwa kuwafuatilia kuwa na uzazi shirikishi i.e Mwalimu, Dereva, Matron, Mzazi na Taaluma.

  Muwe na malezi mema. Sambaza ujumbe huu kuokoa watoto.

  Goodluck Mshana.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku