Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Septemba 16 iligawanya Madiwani wake ambapo baadhi walikwenda Manispaa mpya ya Ubungo na baadhi kubakia Manispaa ya Kinondoni.

Akizungumzia hatua hiyo, Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alsema kuwa uamuzi huo ulifikiwa na Baraza la Madiwani baada ya serikali kuunda wilaya mpya ya Ubungo na Kigamboni. Aidha alisema kuwa mbali na kugawanya Madiwani hao, lakini pia wamegawanya watumishi wengine.

Baada ya majuma mawili tunategemea Wakurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na Ubungo wataitisha uchaguzi ili kuweza kumchagua Meya na Naibu Meya wa Manispaa husika, alieleza Meya wa Kinondoni.

Kufuatia mgawanyo huo, Kinondoni itakuwa na Kata 20 wakati Ubungo itakuwa na Kata 14.


Post a Comment

 
Top