Sep 17, 2016

MATEMBEZI Dar Yakusanya Sh1.5 Bilioni za Waathirika wa Tetemeko Bukoba Kagera

Zaidi ya Sh1.5 zimechangwa katika matembezi maalum yanayofanyika jijini hapa kwa ajili ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi iliyopita.

Kiasi hicho cha fedha kimetokana na ahadi na michango ya fedha za taslim baada ya wadau mbalimbali kuitikia wito wa matembezi hayo yaliyoitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ili kuwachangia wananchi hao waliothiriwa vibaya na tetemeko hilo.

Matembezi hayo ya kilomita tano yameanzia na kumalizikia katika eneo la ufukwe wa Coco jijini hapa na kuongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.

Katika matembezi mengine ya kuwachangia wananchi hao yaliyofanyika katikati ya jiji, Chama cha madalali wa huduma za bima (Tiba) kimetoa hundi ya Sh20 kwa ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuchangia waathirika wa tetemeko hilo lililogharimu maisha ya watu 19 mpaka sasa.

Rais wa Tiba, Mohamed Jaffer amesema kilichotokea Kagera kinapaswa kuwa fundisho kwa watu kuwa na utaratibu wa kukata bima zikiwemo zenye sera ya  kuhudumia walioathiriwa na majanga.

Habari zaidi kukujia ndani ya gazeti la Mwananchi kesho na kwenye epaperBonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR