Sep 17, 2016

MAWAZIRI na Wabunge Watoro Wachimbwa Mkwara

Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameonya kuhusu kuwepo ongezeko la wabunge na mawaziri watoro bungeni.

“Kuna orodha nimeiandaa ya watoro katika kamati, lakini kwa leo sitawataja hapa kwa sababu nimeona tuendelee kuwafuatilia katika vikao vijavyo, kama hawatabadilika nitawaambia waajiri wao, yaani wabunge watoro nitawasema kwa wananchi wao na kwa viongozi wa vyama vyao na kwa mawaziri watoro, nitamwaambia namba moja, kwamba mawaziri hawa hawawajibiki ipasavyo,” alionya Ndungai.

Alisisitiza kutotania katika suala hilo na kuongeza kuwa mahudhurio katika Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 unaotarajiwa kuanza Novemba Mosi mwaka huu, ndio kitakakuwa kipimo chao cha mwisho.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR