Sep 8, 2016

Mbowe 'Serikali Inaonekana Haina Huhakika nini Kinaendelea Katika Uchumi'


Mbowe amefunfuka haya kwenye ukurasa wake wa instagram:

,"Kwa sasa hali ya uchumi inaonekana kuyumba na biashara kudorora,
Nimeitaka Serikali itoe twakimu kuhusu uchumi kushuka. Waziri Mkuu amesema kwa sasa hawana uhakika na hawana takwimu kuhusu hali ya uchumi kudorora na kudai kuwa watakaa na wadau mbalimbali wa Uchumi ili kujua kama uchumi umeyumba kweli.

Swali langu lingine la nyongeza nimemuuliza Waziri Mkuu, Kwa kuwa Kamati ya Bunge ilienda bandarini na kuthibitisha kuwa mizigo imepungua na wadau ambao Serikali inasema itawashirikisha, wenyewe pia wanalalamika kuhusu hali mbaya ya uchumi kwna sasa;Hoteli zimefungwa, Kampuni zimefungwa, watalii wamepungua na Serikali inaonyesha kuwa haina uhakika na nini kinaendelea,

Je ni Serikali imeshindwa kuendesha nchi?"


Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA

Post a Comment

Share:

1 comment:

  1. Mie kwa kweli nimechoka na mbowe kwani hamna kitu cha kufanya? Tuonyesheni basi hata maendeleo mliyoyafanya. Mwacheni rais wetu afanye anayoyaona kuwa yansaidia nchi. Vipaumbele vyenu si vipaumbele vyake. So haiwezekani kuwe na mafahari 2 kwenye zizi moja, nyie tumeshawazoea na kama hamjui Mbowe tumekuchoka kiukweli unatuvuruga tu.

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © Siasa Huru l Habari za Siasa | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by SiasaHuru.com