Mshambuliaji asiye isha visa Mario Balotelli ambaye saivi amesajiliwa na klabu ya Nice ya Ufaransa amesema kujiunga na Liverpool, ‘ulikuwa uamuzi mbaya zaidi aliowahi kuufanya maishani mwake’.

“Isipokuwa mashabiki, ambao hunishabikia, na wachezaji kadhaa ambao tunasikilizana, sipendi klabu yenyewe,”

Balotelli ameiambia runinga ya Ufaransa ya Canal Plus.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alisema hayo kabla ya kufunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza na klabu ya Nice katika michuano ya Ligue 1 walipofunga mabao 3-2 dhidi ya Marseille siku ya Jumapili.


Post a Comment

 
Top