• Breaking News

  Sep 13, 2016

  MCHUNGAJI Awapiga Marufuku Waumini Kujenga Nyumba za Kifahari


  Mchungaji wa Kanisa la Ufunuo maarufu la Mungu wa Bendera wilayani Bukombe Mkoa wa Geita, Heryyabwana Majebele amewapiga marufuku waumini wa kanisa lake kujenga nyumba za kifahari, badala yake waelekeze fedha hizo kwenye elimu ya watoto wao.

  Akizungumza wakati wa ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kuwaepusha waumini wake na wakazi wa Mkoa wa Shinyanga na janga la tetemeko la ardhi lililosababisha maafa mkoani Kagera, Mchungaji Majebele alisema uwekezaji katika elimu ndiyo ukombozi wa Taifa.

  Kuhusu amani na utulivu nchini, Mchungaji Majebele aliwataka Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake kukemea aina yoyote ya uvunjifu wa amani bila kuwaonea haya wanaojaribu kuvunja misingi ya umoja, upendo, mshikamano na kuvumiliana iliyojengwa na waasisi wa Taifa.

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kanisa hilo, Prisca Chando aliliomba kanisa na waumini wote, hasa wanawake kusimama kidete kupiga vita mila na desturi zinazokandamiza watoto wa kike kwenye suala la elimu.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku