• Breaking News

  Sep 4, 2016

  Mgogoro wa Mbowe Hotel Ltd na NHC ni wa Muda Mrefu..

  Mbowe Hotels Ltd iliyokuwa ya baba yake huyu Freeman ilianza kutumia jengo lenye "mgogoro wa kisiasa" mwaka 1973.

  Mwaka 1989 Club Bilcanas ilianzishwa kwenye jengo hilo .Mwaka 1993 Mbowe Hotels wakafanya ukarabati mkubwa wa jengo na Club waliodai uligharimu bilioni 1.3 wakati huo.

  Wakawa na mgogoro wa makubaliano ya umiliki ,NHC wakitaka 50% lakini MHL wakitaka 75% ya umiliki. Historia ni ndefu sana.Sasa ukihangaika kulamba miguu ya wakubwa wako kuingilia mgogoro wa NHC na Mbowe ili upongezwe kwa kumkomoa mtu aliyezaliwa akazikuta pesa, akaziendeleza na kuishi nazo muda wote unakuwa unajilisha upepo.
  Zaidi kwa wale mnashabikia mgogoro huu jilaumuni kwa nini mlizaliwa na wazazi maskini ambao hawakujifunza kujitafutia.

  Mbowe Hotels Ltd ni kampuni na NHC vile vile ,zinaweza kushitaki na kushitakiwa .Ukivamia jambo kwa kumuona Mbowe mtu,hutamuona kupambana naye.Tusubiri ngoma ya mahakamani .Nani atalipa fidia?

  Huu mchezo hautaji hasira.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku